Waziri
Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wanawake waponda kokoto nje ya
kituo cha afya cha Bugarama,na kuwataka wajiorodheshe majina na
kuyapeleka kwa afisa maendeleo wa kata ili.waweze kupatiwa mkopo kwa
ajili ya kununua mashine ya kusaga kokoto.
Akina mama wakiendelea na kazi zao katika eneo hilo.
Waziri
wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto akisalimiana na
wananchi wa kata ya Bulyahulu alipofika kukaguaujenzi wa zahanati.
Waziri
Ummy Mwalimu akiekekeza kitu kwenye jengo hilo la kituo cha afya na
kuahidi ataipa kibali kituo hicho kibadilishwe na kuwa hospitali ya
wilaya ili kuwaounguzia mzigo wananchi wa halmashauri hiyo kwenda kupata
matibabu mjini kahama,kushoto ni mganga mkuu wa wilaya hiyo dkt.Hamad
Nyembea.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa akimuonesha dirisha la dawa Waziri.wa afya,maendeleo ya Jamie,jinsia,wazee na watoto.
Ukaguzi wa ujenzi wa zahanati hiyo ukiendelea
Picha ya pamoja
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Msalala wilayani kahama,amepewa wiki mbili awe
amempatia ripoti waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na
watoto, Ummy Mwalimu ,wanawake wanaoponda kokoto wamewezeshwaa kwa
kupatiwa mkopo wa kiasi gani na mafunzo yapi.
Hali
hiyo imetokea wakati waziri huyo alipofika halmashauri hiyo kukagua
ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya bugarama kinachojengwa na
kampuni ya mgodi wa ACACIA iliopo Bulyahulu na kuwakuta wanawake mbele
ya majengo hayo wakiponda kokoto kwa kutumia vifaa duni na vya mkono
Waziri
Ummy alisema hivi sasa kuna vitendea kazi vya Kisasa na vya bei rahisi
ambayo vitawasaidia wanawake hao kuwarahisishia wanawake kuacha kushinda
masaa kumi wakiponda mawe
“Baada
ya makusanyo ya Mapato ya ndani,mkurugenzi unatakiwa kutenga asilimia 5
kwa ajili ya vikundi vya akina mama na sio vikundi vya kujitafutiza
huko mitaani na vya kujuana”
Waziri
Ummy alisema haiwezekani wanawake wanaojishughulisha na shughuli
ndogondogo wakaachwa pasipo kusaidiwa kwani wanawake wengi ndio
wanaosaidia familia.
“Tusipowawezesha
wanawake hawa,mnataka tuwawezeshe wanawake gani?hawa ndio waliotupigia
kura hawa,lazima tuwaonyeshe maneno ya Rais Magufuli hayakuwa matupu
mana alisema anataka kuwawezesha wanawake na ndo mana kila halmashauri
inatakiwa kutenda asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili hii”
Aidha,alisema
wawahamasishe wanawake wengine katika Kata zote kujiunga kwenye vikundi
hususan wale wanaojituma na kujitoa kwa biashara ndogondogo
wanawake
hao wapatao thelathini wanaoponda kokoto karibu na kituo cha afya
Bugarama walisema wanaomba wanawake wawezeshwe kwani hawajui kama kuna
pesa zinatakiwa kutengwa kwa ajili ya wanawake,hata hivyo walimshukuru
waziri huyo kwa kuwafumbua macho.
Naye
mganga mkuu wa halmashauri hiyo dkt. Hamad Nyembea alisema kampuni hiyo
ya ACACIA ilianza ujenzi wa kituo cha afya julai,2014 na hadi kukamilika
ujenzi huo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7, na ujenzi wa
zahanati ya bulyahulu itagharimu zaidi ya milioni mia tatu
No comments:
Post a Comment