Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima katika uzinduzi wa tawi hilo walisema kwamba hapo awali walilazimika kusafiri kwenda wilaya za Arusha na Babati kutafuta huduma hiyo jambo lililowapelekea usumbufu.Joseph Lulu ambaye ni mkulima wa mboga mboga wilayani humo alisema kwamba kitendo cha
TFA kufungua tawi wilayani hapo kutawapatia nafuu ya na kuwaondolea usumbufu wa gharama na muda kwenda mbali kusaka mbegu na zana za kilimo.Mkulima huyo alisema kwamba hapo awali walilazimika kutafuta bidhaa hizo kwenye minada katika eneo la Endasak wilayani humo jambo ambalo liliwapelekea kununua dawa zisizo na kiwango.“Tumepata nafuu sana kwa hili duka kufunguliwa hapa hapo zamani tulikuwa tukienda Arusha au Babati kutafuta dawa na pembejeo za kilimo”alisema LuluHatahivyo,Ibrahim Anaeli ambaye ni mkulima wa matunda wilayani humo alisema kwamba hapo awali walikuwa wakinunua dawa za kilimo na mifugo zisizokuwa na kiwango kutokana na uelewa duni.Alisema kwamba ufunguzi wa duka hilo utawasaidia kununua dawa zilizothibitishwa na ubora na kupatiwa elimu kabla ya kununua bidhaa hizo na kuisahuri serikali kuyatupia jicho baadhi ya makampuni yanayotengeneza dawa bandia za kilimo na mifugo.“Hapa tumejionea kabla ya kununua dawa wanakupa elimu kwanza hapo awali tulikuwa tukinunua dawa na pembejeo za kilimo ambazo hazina ubora hii itatusaidia katika shughuli zetu”alisema AnaeliAwali akifungua tawi hilo mkuu wa wilaya ya Hanag,Thobias Mwilapwa alisema kwamba aliwataka TFA kuleta mapinduzi ya kilimo wilayani humo kwa kuwapa elimu ya kutosha wateja mbalimbali watakaokuwa wakifika kupata mahitaji katika tawi hilo.Mbali na kupongeza hatua hiyo pia aliwataka TFA kuhakikisha wanauza mbegu za kilimo kulingana na mazingira hali ya maeneo husika na kusisitiza kwamba serikali itashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha wanawafikia wakulima wengi wilayani humo.“Leteni bidhaa zinazokabiliana na maeneo husika lakini shirikianeni na serikali za vijiji katika kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na wafugaji ilimlete mapinduzi ya kilimo hapa Hanag”alisema MwilapwaHatahivyo,Afisa mauzo wa TFA kanda ya kazkazini,Renatus Kauki alisema kwamba lengo la kufungua tawi wilayani humo ni kuhakikisha wanawafikia wakulima na wafugaji kwa urahisi na kusogeza huduma karibu yao.Alisema kwamba jambo linalowatofautisha wao na makampuni mengine ni kuuza bidhaa zenye ubora,gharama nafuu pamoja na kuweka kipaumbele katika kutoa elimu kabla ya kuuza bidhaa zao kwa wateja.Alisisitiza kwamba kwa sasa TFA ina matawi 12 hapa nchini katika mkoa wa Arusha,Kilimanjaro,Tanga,Daresalaam,Morogoro,Iringa, Mafinga,Manyara,Mbeya,Mbozi, Babati na Karatu huku ikiwa na takribani wanachama 4,800.
Sunday, 17 April 2016
TFA YAWAPIGA TAFU WAKULIMA NA WAFUGAJI MKOANI MANYARA.
Labels:
HABARI KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment